Barcelona

Lionel Messi aweka rekodi ya ufungaji mabao katika klabu ya Barcelona

REUTERS/Albert Gea

Lionel Messi ameandika historia katika klabu yake ya soka ya Barcelona katika ligi ya La Liga nchini Uhispani kwa kuwa mfungaji bora wa mabao katika historia ya klabu hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa Messi ameifungia Barcelona magoli 234 tangu alipoanza kuichezea klabu hiyo mwaka 2007 na hivyo amevunja rekodi ya miaka sitini iliyokuwa imewekwa na mchezaji wa zamani Cesar Rodriguez aliyefunga mabao 232 wakati akicheza katika klabu hiyo miaka ya 1950.

Messi ambaye ni raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 ametuzwa mchezaji bora duniani mara mbili mfululizo na ameifungia klabu yake mabao 54 msimu huu.

Kocha wa Barcelona Pep Guardiola amesema Messi anastahili kupongezwa sana kwa jitihadi anazofanya katika klabu hiyo na historia aliyoweka inadhirisha hilo.

Jumanne usiku,Messi alifunga mabao matatu na kuisadia Barcelona kuishinda Granada FC mabao 5 kwa 3.

Barcelona iko katika nafasi ya pili kwa alama 66 katika msururu wa ligi kuu nchini humo Uhispania nyuma ya Real Madrid inaongoza kwa alama 71 wakati nafasi ya tatu ikishikiliwa na Valencia kwa alama 47.