Klabu Bingwa

Matokeo ya michuano ya kuwania kombe la Ulaya

Nembo za timu za FC Barcelona ya Uhispania na AC Milan ya Italia
Nembo za timu za FC Barcelona ya Uhispania na AC Milan ya Italia video-match.fr

Mabingwa wa Ulaya Barcelona ya Uhispania inahitaji kushinda AC Milan ya Italia watakachopocheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp tarehe tatu mwezi ujao, baada ya timu hizo mbili kutoka sare ya kutofungana katika mchuano wa kwanza wa robo fainali jana usiku katika michuano ya kuwania kufuzu kwa nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa hao watetezi licha ya kumiliki mchuano huo, walipoteza nafasi nyingi za kufunga kupitia kwa mshambulizi wake Lionel Messi na wakati Zlatan Ibrahimovic wa AC Milan naye akikosa nafasi tele za kuifungia AC Milan katika uwanja wao wa nyumbani wa San Siro.

Mshindi kati ya Barcelona na AC Milan atakutana na Chelsea ya Uingereza au Benfica ya Ureno katika awamu ya nusu fainali ya michuano hiyo ya kutafuta ubingwa wa klabu bora barani Ulaya.

Katika mchuano mwingine uliochezwa jana, Bayern Munich ya Ujerumai iliianza vema kampeni zake za kutaka kufuzu kwa awamu ya nusu fainali kwa kuichabanga Marseille ya Ufaransa kwa mabao 2 kwa 0.

Mabao ya Bayern munich yalitiwa nyavuni na Mario Gomez na Arjen Robben.

Mshindi katika awamu ya pili ya michuano hii ya robo fainali atacheza na Real Madrid ya Uhispani ambayo hapo awali iliishinda Apoel Nicosia ya Cyprus kwa mabao 3 kwa bila katika mchuano wa kwanza wa robo fainali.

Fainali ya michuano hii itaandaliwa mwezi wa tano mwaka huu mjini Munich nchini Ujerumani.