Hispania

Samwel Eto'o afuta kesi ya Barcelona

Reuters

Mchezaji wa zamani wa Barcelona Samweli Eto'o amefuta kesi madai aliyokuwa amefungua akiidai timu hiyo euro milioni tatu.

Matangazo ya kibiashara

 

Eto'o alikuwa anaidai timu hiyo kutokana na uhamisho wake kutoka Barcelona kwenda Inter Milan mwaka 2010.

Klabu ya Barcelona imesemakuwa imepokea barua kutoka katika mahakama iliyokua ikisikiliza kesi hiyo ikieleza uamuzi huo Eto'o.

Katika kesi hiyo Eto'o alikuwa akidai fidia ya kiasi kingine cha fedha kisichojulikana kutokana na uhamisho huo.

Awali Klabu ya Barcelona iliilipa Inter Milan kitita cha dola za kimarekani milioni 66 kwa ajili ya kumchukua mshambuliaji Milan Zlatan Ibrahimovic fedha ambazo zilijumuisha pia uhamisho wa Eto'o kutoka Barcelona kwenda Inter Milan.

Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Cameroon alikua ni miongoni mwa wachezaji walioleta mafanikio katika klabu ya Barcelona akiifungia magoli 152 kabla hajahamia Inter Milan.

Hata hivyo Eto'o aliihama Inter Milan mwaka uliopita alihamia katika klabu ya Anzhi Makhackala ya Urusi.