TENNIS

Wachezaji Novak Djokovic na Rafael Nadal watinga hatua ya robo fainali

Mcheza tennesi namba mbili kwa ubora, Rafael Nadal
Mcheza tennesi namba mbili kwa ubora, Rafael Nadal © Reuters

Michuano ya tennesi ya Monte Carlo inayotimua vumbi nchini Ufaransa katika jiji la Monaco imeendelea kushika kasi huku wachezaji Rafael Nadal na Novak Djokovic wakitinga hatua ya robo fainali.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye michezo ya hapo jana bingwa nambari moja wa mchezo huo Novak Djokovi alifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kumfunga Alexandr Dolgopolov kwa seti mbili kwa moja kwa matokeo ya 2-6, 6-1 na 6-4 na hivyo kutinga hatua ya robo fainali.

Rafael Nadal alifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kufanikiwa kuchomoza na ushindi dhidi ya Mikhail Kukushkin kwa matokeo ya seti mbili bila kwa matokeo ya 6-1 na 6-1.

Joe Wilfried Tsonga yeye amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kumfunga Fernando Verdasco kwa seti mbili bila kwa matokeo 7-6 na 6-2.

Kwa matokeo hayo Novak Djokovic atacheza na Robin Haase kwenye hatua ya robo fainali wakati Rafael Nadal atacheza na Stanislas Wawrinka kwenye hatua hiyo.