UINGEREZA

Chelsea na Arsenal nguvu sawa

fanpop.com

Timu ya Chelsea ambayo inakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya timu ya Barce Barcelona siku ya Jumanne, jana imetoshana nugvu na timu ya Arsenal katika mchezo uliopigwa katika dimba la Emirates baada ya kutoka sare ya bila kufungana.

Matangazo ya kibiashara

Timu ya Chelsea iliwachezesha wachezaji kadhaa wa akiba ili kujaribu kujiandaa na mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya.

Pamoja na timu zote kupata nafasi nzuri za hapa na pale za kuweza kufunga, mchezo huo ulikosa msisimko mkubwa kutokana na wachezaji kupoteza pasi na mipira mara kwa mara

Kwa matokeo hao Arsenal inasalia katika nafasi ya tatu, ingawa matokeo ya Tottenham na Newcastle huenda yakasababisha mabadiliko na kuipa wasiwasi timu hiyo.