ligi ya mabingwa

Kitim tim leo baina ya Chelsea na Barcelona katika nusu fainali ya pili

Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba na beki wa Barcelona Puyol
Mshambuliaji wa Chelsea Didier Drogba na beki wa Barcelona Puyol

Timu ya FC Barcelona ya Uhispania, inaipokea baadae jioni hii timu ya Chelsea kutoka Uingereza katika nusu fainali ya pili ya marudio kuelekea fainali kuwania klabu bingwa barani Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Katika mechi ya awali, Chelsea ilifaanikiwa kupata ushindi wa bao moja, bao ambalo lilitiwa wavuni na mchezaji wa kimataifa Didier Drogba baada ya kupewa pasi nzuri na mchezaji mwenzake katika ya 46 kuelekea mapunziko ya kipindi cha kwanza.

Barcelona ilijaribu bila mafaanikio kusawazisha bao hilo. Hadi kipenga cha mwisho matokea ilikuwa ni bao moja kwa bila kwa faida ya Chelsea.

Baadae jioni ndipo tutajuwa ni timu ipi ambayo itaibuka mshindi na kuingia fainali kucheza na Real Madrid au Bayern ambazo zitakutana kesho ili kujuwa nani ataibuka mshindi na hivyo kucheza fainali.