Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Roy Hodgson huenda akachukua mikoba ya Fabio Capello kwa ajili ya kuinoa Timu ya Taifa ya Uingereza

Kocha Mkuu wa Klabu ya West Bromwich Albion Roy Hodgson ambaye anatarajiwa kuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza
Kocha Mkuu wa Klabu ya West Bromwich Albion Roy Hodgson ambaye anatarajiwa kuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza
Ujumbe kutoka: Nurdin Selemani Ramadhani
2 Dakika

Chama Cha Soka Nchini Uingereza FA kinaendelea na mazungumzo na Kocha Mkuu wa Klabu ya West Bromwich Albion Roy Hodgson kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Fabio Capello ili aweze kukinoa kikosi cha Timu ya Taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa FA David Bernstein akiwa pamoja na jopo la wataalam wengine wanne kutoka Chama hicho wakizungumza na Hodgson kwa lengo la kumkabidhi jukumu la kuinoa timu hiyo kueleka Michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya.

FA imekuwa ikihaha kuhakikisha inaziba nafasi ya Capello ambaye alisitisha mkataba wake na Uingereza mwezi February kutokana na kuchukizwa na hatua ya kunyang'anywa unahodha kwa John Terry.

Mazungumzo baina ya pande hizo mbili yangalia yanaendelea na iwapo wataafikiana basi Hodgson atachukua jukumu la kuiongoza Uingereza kwenye Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya yatakayofanyika mwezi Juni hadi Julai nchini Poland na Ukraine.

Hodgson ambaye hakupata mafanikio wakati anaifundisha Liverpool tofauti na kile alichovuna wakati anakinoa kikosi cha Fulham na kuifikisha hatua ya Fainali ya Europa alikuwa hapewi nafasi kubwa ya kuchukua kazi hiyo.

Kocha wa Tottenham Harry Redknapp ndiye alikuwa anapigiwa chapuo kwa kiasi kikubwa kuanzia na wachezaji hadi waandishi wa habari lakini inaonekana bahati si yake na sasa Hodgson ndiye ambaye anaweza kuchukua nafasi hiyo.

Hodgson ambaye aliwahi kuifundisha Inter Milan ameonekana anauzoefu mkubwa ukimlinganisha na Redknapp huku nafasi za kufundisha timu za taifa akizipata katika timu za Uswiss, Umoja wa Falme za Kiarabu na Finland.

Rekodi ya Hodgson inaonesha amefanya kazi katika nchi za Sweden, Uingereza, Uswiss, Italia, Denmark na Norway akifundisha ngazi ya Klabu na hata Timu za Taifa kitu ambacho kinampa nafasi zaidi ya kupata nafasi hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.