UINGEREZA

Manchester City yakaribia kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Nchini Uingereza baada ya kuifunga Manchester United

Goli la Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany katika mchezo dhidi ya Manchester United lilitosha kuwapa ushindi na hivyo kukaribia kutwaa Ubingwa msimu huu iwapo watashinda michezo yao miwili ambayo imesalia.

Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany akipiga kichwa mbele ya beki wa Manchester United Chris Smalling na kuipa ushindi timu yake
Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany akipiga kichwa mbele ya beki wa Manchester United Chris Smalling na kuipa ushindi timu yake
Matangazo ya kibiashara

Kompany alifunga goli hilo muda mchache kabla ya mapumziko akiunganisha kona ambayo ilipigwa na David Silva na hivyo kuiweka timu yake katika mazingira mazuzi ya kutwaa ubingwa na kuondoa Manchester United kileleni.

Nahodha huyo wa Manchester City alipiga kichwa baada ya kumzidi ujanja beki wa Manchester United Chris Smalling na kisha mpira huo kumpita golikipa wake David De Gea na kuwapa uongozi hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Manchester City iliendelea kutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa huku Manchester United ikioneka imekwenda Etihad kwa ajili ya kuzuia na kushindwa kabisa kutengeneza nafasi za kutafuta magoli.

Mchezo huo kidogo uingie dosari baada ya makocha Sir Alex Ferguson na Roberto Mancini kurushiana maneno na kumlazimisha mwamuzi wa akiba kuwaamulia kutokana na Sir Ferguson kukerwa na kucheza faulo mshambuliaji wake Danny Welbeck na kiungo wa City Nigel De Jong.

Timu zote zmasalia na michezo miwili kabla ya ligi kumalizika huku Manchester City ikiongoza kwa tofauti ya magoli nane mbele ya Manchester United na iwapo City watateleza basi huenda maajabu yakashuhudiwa.

Kocha wa Manchester City Mancini amesema kuwa bado wanamichezo migumu mbele yao dhidi ya Newcastle United kabla ya kucheza na Queens Park Rangers huku United wakikabiliwa na Swanse na Sunderland.

Sir Ferguson kwa upande wake amesema Manchester City wapo katika nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa msimu huu baada ya ushindi wao wa jana lakini amesema wataendelea kuhakikisha wanashinda michezo yao miwili iliyosalia.