UHISPANIA

Real Madrid yatwaa Kombe la La Liga wakati Messi akifunga magoli matatu kuisaidia Barcelona

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho akiinuliwa juu na wachezaji wake baada ya kufanikiwa kutwaa Ubingwa wa La Liga
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho akiinuliwa juu na wachezaji wake baada ya kufanikiwa kutwaa Ubingwa wa La Liga

Real Madrid imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Nchini Uhispania maarufu kama La Liga na kuwa taji lao la 32 ikiwa imesalia michezo miwili baada ya kuwafunga Athletic Bilbao kwa magoli 3-0.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Real Madrid kwenye mchezo huo ilianikizwa na magoli ya kwake Mshambuliaji wa Kimataifa wa Argentina Gonzalo Higuain, Kiungo wa Ujerumani Mesut Ozil na Mshambulizji mwenye uchu raia wa Ureno Cristiano Ronaldo.

Ubingwa huo nusura uote mbawa kutokana na Ronaldo kukosa mkwaju wa penalty katika za mwanzo wa mchezo na hivyo kuipa timu yake wakati mgumu wa kuanza kutafuta goli la mapema na hivyo alikuwa Higuain aliyefungua milango hiyo.

Ushindi huo umezima kabisa ndoto za Barcelona kutwaa ubingwa msimu huu licha ya ushindi wao wa magoli 4-1 mbele ya Malaga katika mchezo wao wa mapema uliopigwa ugani Nou Camp.

Ubingwa huo wa Real Madrid unamfanya Kocha wake Jose Mourinho kuwa kocha wa kwanza kutwaa ubingwa katika nchi nne tofauti akinzia Ureno akiwa na FC Porto, Uingereza wakati anainoa Chelsea, hali kadhalika Italia wakati anaifunza Inter Milan na sasa akiwa Uhispania.

Wachezaji wa Real Madrid baada ya mchezo huo kila mmoja hakusita kueleza furaha yake baada ya kukosa Ubingwa kwa miaka minne na sasa imekuwa ahueni kwao baada ya kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Bayern Munich.

Katika Mchezo wa mapema huko Nou Camp ulishuhudia Mchezaji Bora Duniani Lionel Messi akiisaidia Barcelona kupata ushindi wa magoli 4-1 huku peke yake akifunga magoli matatu na jingine likikwamishwa nyavuni na Carles Puyol.

Lionel Messi baada ya kufunga magoli hayo matatu ameweka rekodi ya kuwa mchezji ambaye amefunga magoli mengi zaidi kwenye msimu mmoja na kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Gerd Muller.

Kwa matokeo hayo mbio pekee ambazo zimesalia nchini Uhispania ni baina ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ambao wanagombea tuzo ya mfungaji bora huku Messi akimzidi Ronaldo kwa magoli mawili sasa.