UINGEREZA

Mambo yainyookea Man City

Yaya Toure mchezaji aliyeipatia Man City mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United.
Yaya Toure mchezaji aliyeipatia Man City mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United.

Manchester City imejitengenezea njia katika kumalizia ligi kuu ya England na huenda ikatangazwa bingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1968.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Man City unakuja baada ya mchezaji wake Yaya Toure kufunga mabao mawili na kuipatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United.

Zikiwa zimesalia dakika 20 mpira kumalizika Yaya alifanikiwa kuchenga na kutinga nyavuni na kujinyakulia goli maridadi.

Baadae kidogo Yaya Toure akaongeza bao la pili kwa mkwaju wa karibu huku muda nao ukiwa umewatupa mkono Newcastle.

Iwapo Manchester City watafanikiwa kupata ushindi dhidi ya QPR katika mechi ya kumalizia msimu,watatawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya kandanda ya England na kuweka historia tangu mwaka 1968.