LIGI KUU YA UINGEREZA

Bingwa wa ligi kuu ya Uingereza kufahamika Juma lijalo

Kushoto kocha wa Man Utd, Alex Furgeson, katikati kocha wa QPR Mark Hughes, kulia kocha wa Man City, Roberto Mancin
Kushoto kocha wa Man Utd, Alex Furgeson, katikati kocha wa QPR Mark Hughes, kulia kocha wa Man City, Roberto Mancin Reuters

Ligi kuu nchini Uingereza imeendelea mwishoni mwa juma na kushuhudia vinara wawili wa ligi hiyo wanaolinga kwa alama Manchester united na Manchester City zikipata ushindi kwenye mechi zao na hivyo bingwa atajulikana kwenye mechi zao za mwisho.

Matangazo ya kibiashara

Mchezo ambao ulikuwa umevuta hisia za wapenda soka wengi nchini Uingereza na dunia kwa ujumla ulikuwa ni kati ya timu ya Newcastle United waliokuwa wanacheza na Man City mchezo ambao umeshuhudia Man City wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mchezo huo ambo ulikuwa muhimu kwa timu zote mbili, ambapo Newscastle walihitaji ushindi ili kuendelea kuitafuta nafasi ya tatu, wakati Man City walitakiwa kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri zaidi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya nchi hiyo.

Mechi nyingine iliwakutanisha Tottenham Hostspurs ambao walikuwa na kibarua dhidi ya Aston Villa inayopigana kutoshuka daraja.

Mchezo huo meshuhudia Tottenham wakishindwa kukwea hadi kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Aston Villa.

Mchezo mwingine ulizikutanisha timu ya Manchester United ambao walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani wakiwakaribisha vijana wa Swansea kwenye mchezo ambao umeshuhudia Man Utd wakichomoza na ushindi wa mabao 2-0.

Kwa matokeo hayo, ni wazi sasa bingwa wa ligi kuu ya Uingereza atafahamika kwenye michezo ya mwisho itakayopigwa jumapili ijayo ambapo Man Utd watakuwa ugenini kucheza na sunderland wakati Man City watakuwa nyumbani kucheza na QPR.