LIGI KUU YA ITALIA

Juventus, mabingwa wapya wa ligi kuu ya Italia - Seria A

Wachezaji wa timu ya Juventus wakishangilia ubingwa
Wachezaji wa timu ya Juventus wakishangilia ubingwa Reuters

Klabu ya Juventus ya mjini Turin imefanikiwa kutwaa taji la Seria A baada ya kuifunga Calgiari kwa mabao 2-0, huku AC Milan wakipoteza mchezo wao mbele ya Inter Milan kwa mabao 4-2.

Matangazo ya kibiashara

Vibibi vizee vya jiji Turin wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya AC Milan iliyokuwa inapewa nafasi ya kuizua timu hiyo kutwaa taji hilo mapema, kufungwa na Inter Milan kwa mabao 4-2.

Mshambuliaji wa Inter Milan Diego Milito aliifungia timu yake mabao matatu kati ya manne yaliyotosha kabisa kuzamisha jahazi la AC Milan ambao walikuwa na matumaini makubwa ya kutwaa taji hilo.

Juventus ambayo ilinyang'anywa ubingwa wa msimu wa mwaka 2005/2006 baada ya kubainika kupanga matokeo kupata ushindi kuweza kutwaa taji la nchi hiyo na kushushwa daraja.

Taji hili linakuwa ni taji la 28 kuwahi kushikiliwa na klabu hiyo ambapo mashabiki wa timu hiyo kwenye jiji la Turin walifurika kusherekea ubingwa timu yao.