UINGEREZA

Mabondia, Dereck Chisora na David Haye kupanda ulingoni mwezi wa saba mwaka huu

Mabondia David Haye na Dereck Chisora wanatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa tarehe 14 ya mwezi wa July, kwenye pambano ambalo shirikisho la ngumi la Luxembourg limepinga kufanyika.

Bondia Dereck Chisora (Kushoto) na David Haye (kulia) wakati walipokutana mjini Munich
Bondia Dereck Chisora (Kushoto) na David Haye (kulia) wakati walipokutana mjini Munich Reuters
Matangazo ya kibiashara

Meneja wa bondia Chisora, Frank Warren amethibitisha bondia wake kutaka kuzichapa na Haye na kwamba ni lini pambano hilo litapangwa itajulikana baadae hii leo.

Chisora na Haye walirushiana makonde mjini Munich nchini Ujerumani wakati walipokutana nje ya ukumbi wa ngumi ambako Chisora alikuwa amepigana na Vital klitschko na kupigwa.

Chisora alijikuta akinyang'anywa leseni ya kupigana mara baada ya kukabiliana na mpinzani wake nje ya uwanja baada ya shirikisho la ngumi nchini Uingereza kudai kuwa bondia huyo ndie aliyekuwa mchokozi.

Hata hivyo meneja wa Chisora aliamua kukata rufaa kupinga uamuzi wa bondia wake kunyang'anywa leseni wakati kama ni makosa basi Haye nae alipaswa kuhukumiwa kwasababu ndie alieanza kumrushia maneno ya kejeli mwenzake.

Chisora ambaye ameonekana kuwa mtukutu, aliwahi hata kumpiga kibao Klitscko mwenyewe wakati wakipima uzito mjini Munich kabla ya kumwagia maji kaka yake Klitscho, Wladmir.