TENESI

Novak Djokovic asonga mbele kwenye michuano ya Madrid Master

Novak Djokovic mchezaji nambari moja wa mchezo wa Tennesi duniani
Novak Djokovic mchezaji nambari moja wa mchezo wa Tennesi duniani Reuters

Mchezaji nambari moja kwa ubora wa mchezo wa Tennesi, Novak Djokovic ameendelea kudhihirisha umwamba wake kwenye mchezo huo baada ya kufanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya Madrid Master.

Matangazo ya kibiashara

Djokovik amefanikiwa kusonga mbele kwenye hatua inayofuata baada ya kumfunga Daniel Gimeno-traver kwa matokeo ya seti mbili kwa moja kwa matokeo ya 6-2, 2-6 na 6-3.

Kwenye mechi nyingine Tomas Berdych alikuwa na kibarua dhidi ya Kevin Anderson na kufanikiwa kusonga mbele baada ya kumfunga mpinzani wake kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-4 na 4-3.

Mchezaji nambari 10 kwa mchezo huo Juan Martin Del Potro alifanikiwa kusonga mbele baada ya kumshinda mpinzani wake Florian Mayer kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-4 na 6-2.

Kwa upande wa wanawake mchezaji nambari moja kwa mchezo huo Victoria Azarenka alifanikiwa kumsambaratisha mpinzani wake Andrea Hlavackova kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-3 na 7-6.

Kwenye mchezo mwingine, Maria Sharapova alifanikiwa kusonga mbele baada ya kumfunga mpinzani wake Klara Zakopalova seti mbili bila kwa matokeo ya 6-4 na 6-3.