SERIA A

Shirikisho la soka nchini Italia laanzisha uchunguzi dhidi ya vilabu 20 vinavyotuhumiwa kupanga matokeo

Mashabiki wa soka nchini Italia wakiingia uwanjani mara baada ya mchezo
Mashabiki wa soka nchini Italia wakiingia uwanjani mara baada ya mchezo Reuters

Chama cha soka nchini Italia kimetangaza kuanzisha uchunguzi dhidi ya timu zaidi ya 20 kwa tuhuma za kuhusika na njama za upangaji matokeo.

Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la mpira nchini humo limesema kuwa zaidi ya wati 61 watahojiwa wakiwemo wachezaji 52 wa vilabu mbalimbali nchini ambao wanatuhumiwa kuhusika na njama za kupanga matokeo kwenye mechi zao.

Katika ripoti ya shirikisho hilo imesema kuwa tayati watu zaidi ya 30 wamekamatwa na polisi kwa mahojiano kuhusiana na kupanga matokeo kwenye mechi za ligi daraja la kwanza nchini humo.

Uchunguzi huu mpya unakuja wakati ambapo itakumbukwa msimu wa mwaka 2006 timu ya Juventus iliyokuwa kwenye Seria A ilishushwa daraja baada ya kubainika kupanga matokeo.

Ofisi ya mwendesha mashtaka nchini humo imesema kuwa maofisa wake wanachunguza zaidi ya mechi 33 ambazo matokeo yake yanaelezwa kuwa na utata kutokana na baadhi ya timu kuhonga ili kupata ushindi kwenye mechi zao.