EUROPA LEAGUE

Atletico Madrid mabingwa wapya kombe la EUROPA League

Klabu ya Atletico Madrid ya nchini Uhispania imefanikiwa kutwaa taji la kombe la EUROPA league baada ya kuchomoza na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya klabu ya Athletic Bilbao.

Radamel Falcao akishangilia moja ya goli alilofunga
Radamel Falcao akishangilia moja ya goli alilofunga Reuters
Matangazo ya kibiashara

Fainali hiyo ambayo ilipigwa kwenye dimba la National Arena Lia Manoliu mjini Bucharest ilishuhudiwa na mashabiki lukuki wa vilabu hivyo viwili vyote kutoka nchini Uhispania.

Walikuwa ni Atletico Madrid ambao walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 7 ya mchezo bao ambalo lilifungwa na Radamel Falcao ambaye alifanya hivyo tena katika dakika ya 34 ya mchezo

Pambano hilo lilishuhidiwa timu hizo zikienda mapumziko huku Atletico Madrid wakiongoza kwa mabao mawili ambapo katika kipindi cha pili Bilbao walijitahidi kutaka kurejesha bao.

Katika dakika ya 85 Atletico Madrid waliandika bao la tatu na laushindi kupitia kwa Diego na kuzamisha kabisa jahazi la timu ya Bilbao.

Athletic Bilbao ilifika kwenye hatua ya fainali baada ya kuwabania kupita mashetani wekundu wa jiji la Manchester, Manchester United.