TENESI

Nadal na Djokovic watishia kujitoa mashindano ya mwakani ya Madrid wakilalamikia uwanja mbovu

Rafael Nadal (kulia) akiwa na Novak Djokovic (kushoto) wakiwa na vikombe vya kwenye mashindano ya Monte
Rafael Nadal (kulia) akiwa na Novak Djokovic (kushoto) wakiwa na vikombe vya kwenye mashindano ya Monte REUTERS/Olivier Anrigo

Wachezaji Tennesi maarufu duniani Rafael Nadal na Novak Djokovic wametishia kujitoa kushiriki kweny mashindano ya mwakani ya Madrid Master kwa kile walichodai uwanja kutokuwa na kiwango.

Matangazo ya kibiashara

Nadal ambaye ni mchezaji nambari tatu kwa ubora wa mchezo huo duniani, ametishia kujitoa kwenye michuano ya mwakani baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Verdasco kwa kile alichodai uwanja wa Blue umekuwa ukiteleza.

Nadali alipoteza mchezo wake dhidi ya Fernando Verdasco kwa matokeo ya seti mbili kwa moja kwa seti 6-3, 3-6 na 7-5.

Mara baada ya mchezo huo Nadal amedai kuwa sababu kubwa ya yeye kupoteza mchezo huo ilitokana na uwanja kutokuwa kwenye kiwango kinachostahili na mara nyingi alikuwa akiteleza na hivyo kusababisha kupoteza mchezo wake.

Siku ya Jumanne mchezaji Novak Djokovic alitishia kujitoa kwenye michuano hiyo akikosoa waandaji wa uwanja unaotumika mwaka huu na kusema kuwa mashindano yatakuwa magumu kwasababu uwanja unateleza.

Suala hilo pia limegusiwa na Roger Rederer ambaye ametaka waandaji kubadili aina ya uwanja ili kuondoa malalamiko ambayo yamejitokeza.