TANZANIA-ZIMBABWE

Twiga Stars ya Tanzania yalizwa na Zimbabwe

kikosi cha Twiga Stars cha Tanzania
kikosi cha Twiga Stars cha Tanzania

Timu ya soka ya wanawake ya nchini Tanzania imeangukia pua jana mara baada ya kukubali kichapo cha 4-1 toka kwa kina dada wa Zimbabwe katika mchezo wa kimataifa uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Matangazo ya kibiashara

Kipigo hicho kwa Twiga stars ni mara ya pili ambapo awali ilikuwa katika nusu fainali kombe la COSAFA katika mechi iliyochezwa julai 5 mwaka jana jijini Harare ambapo Zimbabwe ilishinda kwa mkwaju wa penati 4-2.

Rufano Machungura alikuwa mwanadada wa kwanza kuandika bao kwa Zimbabwe katika dakika ya tano ya mchezo baada ya walinzi wa Twiga Stars kujisahau.

Mwamuzi wa kimataifa katika mchezo huo Judith Gamba alimtwanga kadi ya njano nyota wa Twiga Fatma Bashir kwa kumchezea vibaya Rufaro.

Mvua imetajwa kuwa changamoto kwani ilichelewesha mchezo huo kuanza baada ya kunyesha kwa wingi jijini Dar es salaam.