Uingereza

Manchester City yamuomba radhi Alex Ferguson

Mchezaji wa Manchester City, Carlos Tevez akiwa na kocha wako, Roberto Mancini
Mchezaji wa Manchester City, Carlos Tevez akiwa na kocha wako, Roberto Mancini REUTERS/Phil Noble

Timu ya Manchester City imemuomba radhi Kocha wa Manchester United ,Alex Ferguson baada ya mchezaji wa Man Cuty, Carlos Tevez kuonesha ishara ya kumkejeli Ferguson wakati wa Shamrashamra za baada ya ushindi wa Man City.

Matangazo ya kibiashara

Tevez alionesha ishara ya kumtaka Ferguson kupumzika kwa amani, ishara ambayo hutolewa kwa walio wafu.

Tamko la Man City limeonesha kusikitishwa sana kitendo cha Tevez na kukiri kuwa alifanya makosa.

Man City imeomba Radhi kwa Kocha huyo na Klabu ya Manchester kwa Ujumla kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na kitendo cha Tevez.

Carlos Tevez mwenyewe amedai kuwa alikuwa amepatwa na Furaha ya hali ya juu wakati huo na hakudhamiria kumdharau Ferguson ambaye anapenda kazi yake.

Tukio hilo linakuja wakati huu wa mwisho wa Msimu wa ligi kuu nchini Uingereza ambao umekuwa wa hatihati nyingi kwa Tevez ambaye alitumia muda wa miezi kadhaa akiwa Nchini Argentina wakati akiwa na tofauti na City ambao ulimgharimu zaidi ya dola za kimarekani milioni 15 kwa ajili ya kulipa faini na kupoteza mapato yake.

Tevez aliondoka United na kujiunga na Man City mwaka 2009 baada ya kutoridhishwa kwake na hali ya kutochezeshwa mechi kadhaa chini ya Ferguson.
 

City iliishinda United kwa tofauti ya Goli moja siku ya Jumapili baada ya kuichapa Queens Park Rangers mabao 3-2.