RWANDA-Tanzania-DRCongo

Umati wajitokeza kumlilia Kiungo wa Club ya Simba Sports Club Patrick Mafisango

Wachezaji wa timu ya Simba Sports Club wakibeba jeneza la mechezaji mwenzao marehemu Patrick mutesa mafisango
Wachezaji wa timu ya Simba Sports Club wakibeba jeneza la mechezaji mwenzao marehemu Patrick mutesa mafisango RFI/BILALI

Maelfu ya watu wamejitokeza jana kwenye viwanja vya TCC Club Chang'ombe jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliekuwa kiungo wa Club ya ya soka ya Simba Sports Club Patrick Mutesa Mafisango raia wa Rwanda mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Vilio, Simanzi na majonzi ndivyo vilivyo tawala katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Rwanda na club ya soko ya Simba Sports Club alifariki usiku wa kuamkia alhamisi mida ya saa kumi na dakika ishirini na tano kutokana na jali ya gari iliotokea katika eneo la Keko jirani na chuo cha Ufundi  VETA jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania.

Mamia ya watu wakiwemo wachezaji na viongozi mbalimbali wa soka na serikali walijitokeza kumuaga Patrick Mutesa Mafisango, akiwemo waziri wa Tanzania wa habari michezo vijana na utamaduni Fenella Mukangura.

Mwili wa mchezaji huyo ambae alikuwa ameitwa kuichezea timu ya taifa ya Rwanda Amavubi umesafirishwa leo asubuhi kwa ndege kuelekea alikozaliwa nchini Jamhuru ya Kidemokrasia ya Congo jwa ajili ya maziko ambapo umeshindikizwa na wachezaji wengine wa timu hiyo.

Mbali na umati mkubwa uliojitokeza kumuaga mchezaji huyo ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wa simba, pia walikuwepo viongozi mbalimbali wa klabu za soka pamoja na vyama vya soka kutoka mikoani nchini Tanzania.