ULAYA

Chelsea mabingwa Ulaya

thesun.co.uk

Kile kindumbwendumbwe cha kusaka klabu bingwa barani Ulaya kimefikia tamati hapo jana huku klabu ya Chelsea ikiibuka kuwa bingwa mpya wa Ulaya kwa mwaka 2012 baada ya kuishinda timu ya Bayern Munich ya Ujerumani kwa mikwaju ya penati 4-3.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika huku timu zote zikitoshana nguvu kwa sare ya goli 1-1 na hivyo kulazimika kwenda katika dakika za nyongeza, timu hizo ziliendelea kuwa sare na hivyo kulazimika kuamliwa kwa mikwaju ya penati.

Awali, Thomas Muller aliiandikia Bayern Munich bao la kwanza katika dakika ya 83, lakini Didier Drogba alisawazisha kwa mpira wa kichwa katika dakika ya 88.

Mchezo uliendelea katika muda wa ziada na dakika nne za kipindi cha kwanza Drogba alimfanyia madhambi Frank Ribery ndani ya eneo la hatari na kusababisha penati ambayo hata hivyo ilidakwa na mlinda mlango Petr Cech.