TANZANIA-MALAWI

Poulsen amteua Kaseja kuwa nahodha wa Tanzania taifa stars.

Kocha wa timu ya Taifa Stars ya Tanzania,Kim Poulsen
Kocha wa timu ya Taifa Stars ya Tanzania,Kim Poulsen in2eastafrica.net

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania Kim Poulsen amemteua kipa Juma Kaseja kama nahodha wa timu hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Kaseja ambaye ni mmoja wa wachezaji wakongwe katika timu hiyo,anachukua nafasi ya Shadrack Nsajigwa ambaye hakujumuishwa katika kikosi cha taifa stars kinachojiandaa kushiriki katika mechi za kusakata tiketi ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Kaseja amesema amefurahishwa mno na uamuzi wa kocha Poulsen na anataumia uzoefu wake wa siku nyingi kama nahodha wa klabu yake ya Simba kuwaongoza wenzake katika timu hiyo.

Taifa stars inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi mwishoni mwa juma hili kabkla ya kumenyana na Cote d voire mwezi ujao jijini Abidjan mwezi ujao.