ITALIA

Nahodha wa Klabu ya Lazio Stefano Mauri akamatwa kwa tuhuma za upangaji wa matokeo na uchezaji wa kamari

Nahodha wa Klabu ya Lazio Stefano Mauri ambaye amekamatwa kwa tuhuma za upangaji wa matokeo na uchezaji wa kamari
Nahodha wa Klabu ya Lazio Stefano Mauri ambaye amekamatwa kwa tuhuma za upangaji wa matokeo na uchezaji wa kamari

Nahodha wa Klabu ya Lazio ya nchini Italia Stefano Mauri pamoja na wachezaji wengine kadhaa wamekamatwa huku Beki wa Timu ya Taifa Domenico Criscito chumba chake kikupekuliwa kwenye kambi ya Tiamu ya taifa ikiwa ni sehemu ya tuhuma za upangaji wa matokeo na uchezaji wa kamari.

Matangazo ya kibiashara

Mauri ni miongoni mwa watu kumi na tisa ambao wanachunguzwa kutokana na kujihusisha na vitendo vya upangaji wa matokeo kwenye ligi ya Italia maarufu zaidi kama Serie A tuhuma ambazo zimeanza kutia dosari ya mchezo wa mpira wa miguu nchini humo.

Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi huo kwa nia ya kuwabaini wale ambao wanatuhumiwa kuchukua hongo kwa ajili ya kupanga matokeo ya michezo matukio yanayohusishwa na wacheza kamari katika nchi hiyo.

Beki wa Timu ya taifa ya Italia Criscito ambaye chumba chake kimepekuliwa ikiwa ni muendelezo wa uchunguzi ambao unafanywa dhidi ya wachezaji wanaotuhumiwa kujihusisha na upangaji huo wa matokeo ikiwa ni sehemu ya kamari inayochezwa zaidi huko Singapore.

Jeshi la Polisi nchini Italia pia limefanya upekuzi kwenye nyumba ya Kocha Mkuu wa Juventus ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Serie A Antonio Conte ambaye kikosi chake kimemaliza ligi bila kufungwa.

Mchezaji mwingine ambaye amekutana na kadhia mchezaji wa zamani wa Genoa na Fiorentina Omar Milanetto mwenye umri wa miaka 36 ambaye kwa sasa anakipiga kwenye Serie B katika kabla ya Pavoda ambaye naye amekamatwa.

Nahodha wa Klabu ya Chievo Sergio Pellissier naye nyumba yake imepekuliwa wakati huu ambapo Jeshi la Polisi likiendelea na msako wa wale wote ambao wamehusika kwa namna moja au nyingine na upangaji wa matokeo.

Watu kumi na tisa hadi sasa wanatuhumiwa kutokana na upangaji huo wa matokeo sanjari na uchezaji wa kamari huku watu kumi na wanne wakiwa wameshakamatwa huku watatu kati yao wakiwa kwenye kifungo cha nyumbani huku wengine wawili wakitakiwa kujisalimisha wenyewe Kituo Cha Polisi.