CAMEROON

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Cameroon kuanza kupata bonasi wakishinda michezo yao ya kufuzu Kombe la Dunia

Kikosi Cha Timu ya Taifa ya Cameroon ambacho kilishiriki kwenye Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010
Kikosi Cha Timu ya Taifa ya Cameroon ambacho kilishiriki kwenye Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2010

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Cameroon wanatarajiwa kuanza kupata bonusi ambayo imetengzwa na serikali kila watakapokuwa wanashinda kwenye michezo yao kwa ajili ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la mwaka 2014.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa serikali unakuja baada ya mgomo ambao uliongozwa na Nahodha wa Timu ya Taifa Samuel Eto'o ambaye baadaye alifungiwa kutokana na kuhamasisha wachezaji kugomea mchezo wa kirafiki wakitaka kulipwa marupurupu.

Serikali ya Cameroon imesema itakuwa inamlipa kila mchezaji dola za kimarekani 9,550 kila watakapokuwa wanashinda mchezo wao wowote wa kufuzu kwenye Kombe la Dunia la mwaka 2014 ambalo litafanyika nchini Brazil.

Wizara ya Michezo nchini Cameroon imethibitisha kuwa tayari kutoa kitita hicho na kila mchezaji ambaye ataitwa kwenye Timu ya taifa atalipwa 500, 000 ya Francs za nchi hiyo ili kuongeza morari yao ya kufanyakazi.

Serikali imesema inataka kuhakikisha Timu ya Taifa ya Cameroon inafuzu kwenye Kombe la Dunia na Kombe la Mataifa ya Afrika ambayo yatafanyika mwakani nchini Afrika Kusini na kufanya vizuri kwenye mashindano hayo yote.

Wizara ya Michezo imesema iwapo Timu ya Taifa itafuzu kwenye mashindano yote watatoa bonusi kubwa zaidia ambayo itaamuliwa na serikali kwa kila mchezaji ambaye amefinikisha timu kufuzu.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Cameroon walikuwa wanaingia kwenye mgogoro na serikali kutokana na kutokuwa tayari kuwalipa fedha ambazo walikuwa wanaahidi kuzitoa kitu ambacho kilikuwa kinachochea mtafaruku wa mara kwa mara.