UFARANSA

Claudio Ranieri apewa mkataba wa miaka miwili kuinoa Klabu ya Monaco ya Ufaransa

Kocha Mkuu wa Klabu ya Monaco Claudio Ranieri aliyepewa kibarua cha kuirejesha klabu hiyo kwenye Ligi Kuu nchini Ufaransa
Kocha Mkuu wa Klabu ya Monaco Claudio Ranieri aliyepewa kibarua cha kuirejesha klabu hiyo kwenye Ligi Kuu nchini Ufaransa © Reuters

Kocha wa zamani wa Klabu za Chelsea, Juventus na Inter Milan Claudio Ranieri amechaguliwa kuinoa Monaco ambayo kwa sasa ipo daraja la pili kwenye Ligi nchini Ufaransa na inapambana kupanda daraja. Ranieri mwenye umei wa miaka sitini amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuinoa Monaco ambayo kwa sasa ipo chini ya Bodi maarufu ya matajiri ambao wamejiapiza kuhakikisha inareje Ligi Kuu nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo raia wa Italia anaanza kazi yake mara moja na hiki kinakuwa kibarua chake cha kwanza tangu atimuliwe na Inter Milan baada ya kuondolewa kwenye hatua ya Mtoano wa Ligi ya Mabingwa katika Mchezo dhidi ya Olympique Marseille.

Mtandao wa Klabu ya Monaco umethibitisha kuingia mkataba na Ranieri ambaye amepewa jukumu la kuirejesha katika Ligi Kuu Monaco ambaye iliteremka daraja msimu uliopita ambao ulikuwa mbaya kwao.

Klabu ya Monaco imesema jopo la watu wenye maamuzi wamediriki kuingia mkataba na Ranieri wakiamini ni mtu mwenye uzoefu mkubwa ambao utasaidia kuijenga timu hiyo na kurejea kwenye kilele cha mafanikio.

Monaco ambao walifanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Ligi ya mwaka elfu mbili na nne na kuambulia kichapo mbele ya FC Porto ilionekana kupoteza mwelekeo wa kufanya vizuri na matokeo yake ikajikuta inashuka daraja.

Ranieri anakabidhiwa jukumu hilo huku naye akiwa hana rekodi nzuri katika za hivi karibuni kutokana na kukumbwa na zimwi la kutimuliwa kwenye Klabu ambazo anazifundishwa kutokana na kushindwa kufikia malengo ya matajiri.