ITALIA-UKRAINE-POLAND

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Italia Balotelli asema hatozumilia vitendo vya ubaguzi atakavyofanyiwa kwenye Euro 2012

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia na Klabu ya Manchester City Mario Balotelli ambaye amejiapiza kupambana na vitendo vya ubaguzi kwenye Euro 2012
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia na Klabu ya Manchester City Mario Balotelli ambaye amejiapiza kupambana na vitendo vya ubaguzi kwenye Euro 2012

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Italia anayekipiga katika Klabu ya Manchester City Mario Balotelli ametishia ataondoka uwanjani iwapo kutakuwa na vitendo vyovyote vya kibagauzi ambavyo vitafanywa dhidi yake kwenye Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ya mwaka 2012 ambayo yatafanyika nchini Ukraine na Poland.

Matangazo ya kibiashara

Balotelli ametishia hata kumtoa mtu roho iwapo atathubutu kumrushia ndizi ikiwa ni sehemu ya vitendo vya kibaguzi ambavyo vimekuwa vikifanywa dhidi ya wachezaji wenye asili ya Afrika wakiwa wanatumika nchi mbalimbali za Ulaya.

Mchezaji huyo mtukutu amesema iwapo akiwa kwenye mitaa halafu mtu akimrushia ndizi anasema atakuwa tayari kufungwa kwani hatoweza kuhimili kuzumilia vitendo kama hivyo dhidi yake.

Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Italia amesema kwake yeye ubaguzi hauna nafasi kabisa na hawezi kuvumilia vitendo vya aina hiyo vifanywe dhidi yake anakabiliana navyo ili kuonesha hasira alizonazo dhidi ya matukio kama hayo.

Balotelli amekuwa muathirika mkubwa wa vitendo vya kibaguzi akiwa na anaichezea Timu yake ya Italia na mwenyewe anasema uvumilivu wake ufika mwisho dhidi ya vitendo kama ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa dhidi yake.

Mshambuliaji huyo ambaye mara zota hakosi vibweka awapo uwanjani amesema imefika wakati ambapo mchezo wa mpira wa miguu uepukane na vitendo vya ubaguzi wa rangi vinavyoanza kuota mizizi kwa sasa.

Kabla ya kuanza kwa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya maarufu kama Euro 2012 ambayo yataanza kutimua vumbi juma lijalo tayari kumeanza kutolewa kwa tahadhari ya uwepo wa vitendo vya ubaguzi wa rangi.

Msimu huu umeshuhudia matukio ya kibaguzi yakijidhihirisha kwenye soka huku nchini Uingereza Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez akifungiwa kwa kufanya vitndo hivyo dhidi ya Beki wa Manchester United Patrice Evra huku Nahodha wa Chelsea John Terry akisubiri kupanda kizimbani kwa vitendo kama hivyo dhidi ya Anton Ferdinand.