UINGEREZA

Brendan Rodgers akubaliana na Liverpool kuiweza kuinoa kwa miaka mitatu

Kocha wa Klabu ya Swansea City Brendan Rodgers ambaye amekubaliana na Uongozi wa Liverpool kuinoa kwa miaka mitatu
Kocha wa Klabu ya Swansea City Brendan Rodgers ambaye amekubaliana na Uongozi wa Liverpool kuinoa kwa miaka mitatu

Klabu ya Liverpool imefikia makubaliano na Kocha wa Swansea City Brendan Rodgers kuchukua jukumu la kuinoa kwa mkataba wa miaka mitatu kuchukua nafasi ya Kenny Dalglish ambaye alitimuliwa baada ya kushindwa kuipatia timu yake nafasi ya kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa.

Matangazo ya kibiashara

Liverpool inatarajiwa kuthibitisha rasmi taarifa hizo za kuingia mkataba wa miaka mitatu na Rodgers mwenye umri wa miaka thelathini na tisa baadaye hii leo baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina ya wamiliki wa timu hiyo na Kocha huyo ambaye amepata mafanikio akiwa na Swansea City.

Liverpool imeridhia kulipa fidia kati ya £4 milioni na £5 milioni kwa Klabu ya Swansea ili kuweza kupata huduma ya Rodgers ambaye alikuwa bado na mkataba wa kuinoa timu hiyo na hivyo Vijogoo Vya Jiji vinalazimika kuvunja mkataba huo.

Rodgers ambaye ni rais wa Ireland ameonekana chaguo sahihi kwa Liverpool huku mashabiki wa timu hiyo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kufungwa goli moja kwa bila na Swansea katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

Liverpool ilitajwa kuwa na mkakati wa kuwanasa makocha kadhaa akiwemo Roberto Martinez ambaye anainoa Wigan Athletic, Kocha wa zamani wa Chelsea Andre Villas-Boas, Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ua Uingereza Fabio Capello pamoja na Kocha ya Ajax Frank de Boer.

Rodgers alivithibitisha vyombo vya habari nchini Uingereza yupo kwenye mazungumzo na Uongozi wa Liverpool siku kumi na mbili zilizopita japokuwa klabu hiyo ilikuwa inasema inaendelea kumsaka Martinez kutoka Wigan.

Liverpool imekuwa na msimu mbaya sana na kujikuta ikimaliza katika nafasi ya nane licha ya kufanikiwa kutwaa Kombe la Caraling na kucheza fainali ya Kombe la Chama Cha Soka FA lakini ikiwa pointi kumi na saba nyuma ya eneo la kufuzu kwa Kombe la Mabingwa Barani Ulaya.

Mafanikio makubwa ambayo ameyapata Rodgers tangu aanze kuifundisha Swansea ameweza kuipandisha daraja na kucheza Ligi Kuu Nchini Uingereza na kisha kuiongoza kuweza kumaliza katika nafasi ya kumi na moja kwenye Ligi msimu huu.