Ufaransa

Michuano ya Tennis ya French Open yazidi kushika kasi

Reuters/Benoit Tessier

Mechi za kufuzu kwa robo fainali ya makala ya mwaka huu ya mchezo wa Tennis ya French Open zinaendelea huku wachambuzi wa mchezo huo wakisema wanatarajia michuano migumu zaidi katika awamu ya robo fainali na nusu fainali.

Matangazo ya kibiashara

Jo Wilfried Tsonga raia wa Ufaransa anayeorodheswa wa tano duniani kwa upande wa wanaume,amemshinda Stanislas Wawrinka kutoka Uswizi kwa seti tano za 6-4, 7-6 (8/6), 3-6, 3-6, 6-4 na kufanikiwa kufika katika robo fainali.

Tsonga sasa atakabiliana na Novak Djokovi wa Serbia anayeorodheswa wa kwanza duniani.

Katika mchuano mwingine uliochezwa siku ya Jumatatu,David Ferrer kutoka Uhispania alimshinda raia mwenzake Marcel Granollers pia kwa seti tatu za 6-3, 6-2, 6-0.

Juan Martin del Potro kutoka Argetina  amemshinda Thomas Berdych kutoka Jamhuri ya Czech kwa seti tano za 7-6 (8/6), 1-6, 6-3, 7-5.

Wachambuzi wa mchezo wa Tennis wanasema makala ya mwaka huu ni magumu mno na wachezaji wenye majina makubwa kama Rafael Nadal na Novak Djokovich huenda  wakapata wakati mgumu wa kusonga mbele katika kinyanganyiro hicho.