FRENCH OPEN

Li Na asema hataki kucheza Tennis kwa sasa

Mchezaji wa kimataifa wa mchezo wa Tennis raia wa Uchina Li Na anasema hataki kucheza tena mchezo huo kwa muda baada ya kushindwa kufanya vizuri katika mashindano ya wazi ya French Open yanayoendelea.

Matangazo ya kibiashara

Li Na dada mwenye umri wa miaka 30 amekuwa akitoa ushawishi mkubwa kwa wasichana wengine nchini Uchina kujitosa katika mchezo wa Tennis.

Baada ya kuchabangwa na mchezaji chipukizi Yaroslava Shvedova kutoka nchini Kazikistan, Li amesema hataki hata kuonekana barani Ulaya na hana mpango wa kuanza kufanya mazoezi ya maandalizi ya michuano ya Wibledon yatakayofanyika Birmingham nchini Uingereza.

Mwaka uliopita Li Na aliweka historia baada ya kushinda ubingwa wa taji hilo la French Open na kuwa mchezaji wa kwanza kutoka barani Asia kunyakua taji hilo.

Katika hatua nyingine gwiji wa nchezo huo duniani Maria Sharapova raia wa Urusi atamenyana na Yaroslava kutoka Kazikistan Jumatabo hii katika awamu ya nusu fainali.

Miongoni mwa wachezaji chipupikizi ambao wameondolewa katika mashindano hayo mbali na Li Na bingwa mtetezi ni pamoja na Victoria Azarenka na Serena Williams.