Manchester United

Manchester United yamsajili Shinji Kagawa kutoka Borussia Dortmound

Klabu ya soka ya Uingereza, Manchester United imekubali kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa.

Matangazo ya kibiashara

Kagawa mwenye umri wa miaka 23 amekuwa akichezea soka yake kulipwa katika klabu ya Ujerumani ya Borussia Dortmound.

Mchezaji huyo tayari amepata kibali cha kufanya kazi na madaktari wa klabu hiyo wamethibitisha kuwa hali yake ya afya ni nzuri.

Kagawa amesajiliwa  kwa Pauni Milioni 12 kutokana na kile klabu ya Manchester United inasema mchezaji huyo ameonesha kiwango cha juu cha soka nchini Ujerumani.

Kati ya mechi 31 ambazo Kagawa amecheza katika ligi ya Ujerumani,amefunga mabao 13 katika msimu wa ligi kuu mwaka uliopita.

Manchester United pia ilitarajiwa  kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Eden Hazard ambaye aliamua kwenda kuichezea klabu ya Chelsea.

Machster United walimaliza katika nafasi ya pili katika ligi kuu ya soka msimu uliopita.