Afrika Kusini

Pitso Mosimane afutwa kazi kama kocha wa Bafana Bafana

Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini limemfuta kazi kocha wa timu ya taifa , Pitso Mosimane baada ya Bafana Bafana kutoka sare ya bao 1 kwa 1 na Ethiopia katika mechi ya kwanza ya kufuzu katika kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Shirikisho hilo limetangaza kuwa,naibu mkufunzi na nahodha wa zamani wa Bafana Bafana Steve Komphela atachukua mikoba ya Mosimane ili kuanza maadaliazi ya timu hiyo inayojiandaa kumenyana na Botswana mwishoni mwa juma hili katika mchuano wa pili wa kufuzu kwa kombe la dunia.

Tangu kujiuzulu kwa Carlos Alberto Pereira raia wa Brazil baada ya kuiongoza Bafabafana katika kombe la dunia mwaka 2010, kiwango cha timu hiyo kimeonekana kushuka tangu Mosimane mwenye umri wa miaka 47 alipoanza kukinoa kikosi hicho.

Katika mechi 7 ambazo Afrika Kusini imecheza, tangu mwezi Agosti mwaka uliopita chini ya kocha Mosimane hawajashinda hata mchuano mmoja.

Afrika Kusini wamejumuishwa katika kundi moja na Ethiopia,Botswana na Jamhuri ya Afrika ya Kati.