FIFA

Ivory Coast timu bora barani Afrika katika mchezo wa soka

Timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast ndio timu bora barani Afrika na ya 16 duniani kulingana na orodha ya hivi punde ya FIFA iliyotolewa siku ya Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Black Stars ya Ghana ni ya pili wakati ikishikilia nafasi ya 25 duniani wakati Algeria ikifunga tatu bora.

Katika kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Uganda Cranes bado inaongoza ikiwa katika nafasi ya 23 barani Afrika na 94 duniani wakati  Kenya ambayo inashikilia nafasi ya 29 barani Afrika na ya 111 duniani ikiwa ya pili .

Amavubi Stars ya Rwanda ni tatu,na ya 35 Afrika na ya 119 duniani ,wakati burundi ikiwa ya nne na ya 40 barani Afrika na ya 131 duniani.

Tanzania ni ya mwisho, na inashika nafasi ya 42 barani Afrika na ya 139 duniani.

Uhispania bado inaongoza orodha ya taifa bora duniani ikifuatwa na Uruguay na Ujerumani mtawalia.

Orodha hii imetolewa baada ya kuchezwa kwa mechi 115 zinazotambuliwa na shirikisho hilo la soka duniani FIFA, huku mechi nyingi zikiwa ni za kufuzu kwa fainali ya kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.

Mechi zingine za kufuzu kwa fainali hizo zimeratibiwa mwishoni mwa wiki hii na huenda ubora wa timu hizo ukabadilika.