Ufaransa

Kocha wa timu ya soka ya Ufaransa Laurent Blanc asema safu yake ya ulinzi inavuja

Ufaransa imeendeleza rekodi ya kutofungwa katika mechi 21 ambazo imecheza baada ya kuishinda Estonia mabao 4 kwa 0 katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, kocha wa Ufaransa Laurent Blanc amesema licha ya ushindi wa mara kwa mara wa vijana wake wwa Le Blue,bado wana tatizo katika safu ya ulinzi suala ambalo ansema analishughulikia kabla ya kuanza kwa mechi za kuwania ubingwa wa Ulaya, Ijumaa hii nchini Ukraine na Poland.

Karim Benzema,Franck Ribbery na Samir Nasir ni baadhi ya wachezaji ambao wameonesha kiwango cha juu cha usakataji wa kabumbu kabla ya kuanza kwa michuano hiyo na kusifa na kocha Blanc.

Ufaransa itafungua mechi yake dhidi ya Uingereza siku ya Jumatatu,na imejumuishwa pamoja na Sweden na wenyeji Ukraine katika kundi moja.

Siku ya Ijumaa mchuano wa ufunguzi utakuwa kati ya wenyeji Poland na Ugiriki,huku Urusi ikicheza na Jamhuri ya Czech.