Ufaransa

Novak Djokovic kumenyana na Roger Federer katika nusu fainali ya French Open

Novak Djokovic na Roger Federer
Novak Djokovic na Roger Federer

Novak Djokovic raia wa Serbia anayeorodheswa wa mchezaji nambari moja duniani katika mchezo wa Tennis kwa upande wa wanaume amefuzu katika nusu fainali ya makala ya mwaka huu ya French Open baada ya kumshinda Jo-Wilfried Tsonga raia wa Ufaransa akiwa nyumbani kwa seti 5 kwa 0 za 6-1, 5-7, 5-7, 7-6 (8/6), 6-1 .

Matangazo ya kibiashara

Roger Federer naye anayeorodhswa wa tatu amefuzu katika awamu hiyo baada ya kumchabanga Juan Martin del Potro raia wa Argentina pia kwa seti 5 kwa 0 za 3-6, 6-7 (4/7), 6-2, 6-0, 6-3.

Baada ya kushinda mashindano ya Wilmbledon nchini Uingereza , US Open na Australian Open,Djokovic anatafuta ushindi wa taji hilo la French Open mwaka huu.

Novak Djokovic na Roger Federer watamenyana katika nusu fainali hiyo siku ya Ijumaa na mshindi huenda akakabiliana na Rafael Nadal katika fainali ya itakayochezwa siku ya Jumapili.

Nadal ameshinda taji la French Open mara tatu mfululizo.