TENNIS-FRENCH OPEN

Mashindano ya kimataifa ya Tennis ya French Open yatinga nusu fainali

Mvua kubwa jijini Paris nchini Ufaransa ilichelewesha kuanza kwa nusu fainali ya makala ya mwaka huu ya mchezo wa Tennis ya French Open kati ya Samantha Stosur kutoka Australia na Sara Errani wa talia.

Matangazo ya kibiashara

Nusu fainali nyingine ambayo pia imecheleweshwa ni kati ya Maria Sharapova anayepewa nafasi kubwa ya kushinda taji hilo dhidi ya bingwa wa taji la Wimbledon Petra Kvitova.

Katika nusu fainali ya wanaume Ijumaa hii, Rafel Nadal na David Ferrer wote kutoka Uhispania watamenyana katika mchuano unaotarajiwa kuwa mgumu.

Rafael Nadal ndiye bingwa mtetezi wa mashindano haya ya French Open kwa upande wa wanaume na alimshinda Nicolas Almagro,kwa seti 3 kwa 0 za  7-6 (4), 6-2, 6-3, huku Ferrer akimshinda Andy Murray kutoka Uingereza kwa seti 4 kwa 0 za  6-4, 6-7 (3), 6-3, 6-2.

Nusu fainali ya pili ni kati ya Mserbia Novak Djokovic ambaye anaorodheswa mchezaji bora duniani katika mchezo huu kwa upande wa wanaume dhidi ya Roger Federer kutoka Uswizi.

Rafael Nadal anasema anataka kuweka rekodi ya kushinda taji la French Open mara 7 na kufikia kiwango cha Bjorn Borg wa Sweden.