POLAND-EURO 2012

Mashindano ya soka ya bara la Ulaya kuanza nchini Poland na Ukraine

Makala ya mwaka 2012 ya soka ya kutafuta bingwa wa bara la Ulaya yaaanza Ijumaa usiku nchini Poland.

Matangazo ya kibiashara

Wenyeji Poland wanafungua dimba dhidi ya Ugiriki katika uwanja wa taifa wa Warsaw katika mashindano hayo yanayoyakutanisha mataifa 16.

Poland watakuwa wanacheza mechi yao ya ufunguzi mbele ya mashabiki wa nyumbani wakisaka ushindi , huku Ugiriki nao ambao wamekuwa wakikabiliana na hali ngumu ya kiuchumi wakitaka kuwadhirishia wapenzi wa soka kuwa wao ni moto wa kuotea mbali.

Poland imejumuishwa katika kundi moja na Urusi na Jahmuri ya Czech ,kipute ambacho Uhispiania ambao ni mabingwa watetezi wanasema wanataka kunyakua tena ubingwa huo baada ya kuishinda Ujerumani mwaka 2008.

Haya ndio mashindano ya kwanza kuandaliwa na mataifa mawili ambapo Ukraine watafungua mchuano wao dhidi ya Sweden siku ya Jumatatu juma lijalo na wamejumuishwa katika kundi moja na Ufaransa na Uingereza.

Suala la ubaguzi wa rangi katika mashindano haya linaedelea kuzungumziwa na kuzua mjadala mkubwa, baada ya maafisa wa timu ya taifa ya Uholanzi kuripoti visa vya ubaguzi wa rangi kwa kile wanachosema wachezaji wao wameimbiwa nyimbo za kuwabagua na mashabiki wa soka nchini Poland.

Maafisa wa soka wa Uholanzi wanasema wamewafahamisha viongozi wa shirikisho la soka barani Ulaya, UEFA kuhusu tukio hilo.