Brazil 2014

Uganda Cranes kuwakaribisha Teranga Lions ya Senegal katika mchuano wa kufuzu kwa kombe la dunia nchini Brazil 2014

Timu ya soka ya Uganda, Uganda Cranes iko nyumbani Jumamosi hii  katika uwanja wa kimataifa wa Namboole jijini Kampala kumenyana na Teranga Lions ya Senegal katika mechi ya mzunguko wa pili ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Uganda Cranes ilianza kampeni yake kwa kupata sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya Angola mjini Luanda mwishoni mwa Juma lililopita.

Senegal nao waliwashida Liberia mabao 3 kwa 1 na wanatakuwa wanacheza mechi ya Jumamosi wakiwa na matatarajio ya kuendeleza ushindi huo.

Uganda Cranes wakiwa mbele ya mashabiki wake wa nyumbani nao watakuwa wanatafuta ushindi wao wa kwanza ,baada ya kukosa nafasi ya kushiriki katika fainali za kombe la mataifa bingwa barani Afrika nchini Gabon na Equirorial Guinea mwaka uliopita.

Harambee Stars ya Kenya nayo itakuwa mjini Windhoek kumenyana na Namibia baada ya kutoka sare ya kutofungana na Malawi Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi.

Timu nyingine katika kundi hilo, Nigeria itamenyana na Malawi mjini Blantyre baada ya kuishindi Namibia bao 1 kwa 0 nyumbani kwao.

Taifa Stars ya Tanzania nayo itaikaribisha Gambia siku ya Jumamosi katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam baada ya kufungwa na miamba wa soka barani Afrika Cote Dvoire mabao 2 kwa 0 mjini Abdjan.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilipoteza bao 1 kwa 0 dhidi ya Cameroon itaikaribisha Togo mjini Kinsasha, wakati Rwanda ikimenyana na Benin jijii Kigali.

Mataifa 10 ya Afrika yatafuzu katika mzungunko wa tatu kutafuta timu 5 zitakazowakilisha bara la Afrika katika kindubwendubwe hicho.