TANZANIA-GAMBIA

Stars ya Tanzania kuivaa Gambia katika kusaka tiketi ya Fainali za kombe la dunia 2014,Brazil

Kikosi cha Tanzania Taifa stars ambacho leo kitaivaa timu ya taifa ya Gambia
Kikosi cha Tanzania Taifa stars ambacho leo kitaivaa timu ya taifa ya Gambia AFP

Timu ya taifa ya nchini Tanzania,Taifa Stars inataraji kushuka dimbani jijini Dar es salaam kucheza na Gambia katika mchezo wao wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia zitakazofanyikia nchini Brazil mwaka 2014.

Matangazo ya kibiashara

Taifa Stars imeshapoteza mechi yao dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa juma lililopita ambapo walifungwa magoli 2-0.

Kocha mkuu wa timu ya Gambia Luciano Machini ambaye anauwezo na uzoefu wa kufundisha timu za Afrika anaona kuwa Stars ina kikosi makini na anatarajia kuona mpambano wa aina yake kati ya kikosi hicho na kile cha Gambia ambacho anakinoa.

Mashabiki mbalimbali wa kandanda kutoka Gabia na Tanzania wamejipanga kujitokeza katika kipute hicho ambacho kitaamua nani ni nani baada ya dakika 90 za mchezo kukamilika.