Ufaransa-Uingereza

Ufaransa kuchuana na Uingereza michuano ya Euro 2012

Wachezaji wa ufaransa wakiwa mazoezini jana Juni 10
Wachezaji wa ufaransa wakiwa mazoezini jana Juni 10 REUTERS/Nigel Roddis

Timu ya taifa ya Ufaransa inashuka uwanjani jumatatu hii kupepetana na Uingereza katika michauo ya kombe la Ulaya inayoendelea nchini Ukraine Polande. Vijana wa Laurent Blanc wamesema wapo tayari kupambana kuhakikisha wanaibuka washindi katika mechi yao hiyo ya kwanza katika michuano hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati Ufaransa wanakutana na Uingereza, wenyeji wa michuano hiyo Ukraine wataipokea Sweden katika mechi ya pili. Hapo jana Italia ilikwenda sare ya kufungana bao moja kwa moja na Uhispania