Euro 2012

Ujerumani yajiweka sawa, huku Uholanzi ikishindwa kuwika

Mshambuliaji wa Ureno Christiano Ronaldo akikabiliana na beki wa Ujerumani
Mshambuliaji wa Ureno Christiano Ronaldo akikabiliana na beki wa Ujerumani courrier-picard.fr

Uholanzi imeshindwa kutumia nafasi 28 walizotegeneza na hivo kujikuta ikifungwa 1-0 na Denmark, huku Ujerumani wakithibitisha ubabe wao kwa kuichapa Ureno 1-0.

Matangazo ya kibiashara

Uholanzi walitegeneza nafasi 28 kwenye uwanja wa Metalist mjini Kharkiv, lakini walishindwa kufunga zaidi ya kuchapwa 1-0 na Denmark matokeo yanayowaacha kwenye wakati mgumu katika Kundi B.

Michael Krohn-Delhi alifunga bao pekee kwa Denmark dakika ya 24, kama ilivyokuwa katika mji wa Lviv ambako Mario Gomez alifunga kwa kichwa goli kwa Ujerumani lililowafanya kuongoza kundi hilo kwa pointi tatu pamoja na Denmark.

Mechi hizo mbili za Jumamosi zilivuta hisia za watu wengi, pia kulishudia Uholanzi wakiweka rekodi ya kumchezesha chipukizi wa miaka 18, Jetro Willems ambaye amekuwa mchezaji wa kwanza mdogo kucheza michuano hiyo.

Kwa matokeo hayo sasa Uholanzi watalazimika kupiga hadi dakika ya mwisho ili wasipoteze mchezo wao ujao dhidi ya Ujerumani utakaofanyika jijini Kharkiv.

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Gomez alifunga bao lake dakika ya 72 na kuwazima Ureno na Ronaldo aliyeshindwa kuonyesha makali yake ya Real Madrid.