Euro 2012

Kocha wa ufaransa Laurent Blanc asema hana hofu ya kucheza na wenyeji wa michuano ya Euro Ukraine

Franck Ribéry y Mathieu Valbuena na Laurent Blanc
Franck Ribéry y Mathieu Valbuena na Laurent Blanc Reuters

Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Laurent Blanc amesema timu yake imejipanga vizuri kuhakikisha inatwaa ushindi katika mechi ya kesho na wenyeji wa michuano ya Euro Ukraine.

Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo amesema mechi yao ya kwanza ya michuano hiyo dhidi ya Uingereza walitoka sare ya bao moja kwa moja matokeo ambayo sio mazuri, lakini timu yake ilicheza vizuri, na wamekuwa wakiuangalia mchezo huo mara kwa mara na kuusoma zaidi ambapo itawasaidia katika mechi yao na wenyeji Ukraine.

Blanc amesema kwamba hana hofu ya kucheza na timu ambayo ipo nyumboni.

Katika hatuwa nyingine ya michuano ya Euro 2012 leo Italia inachuana na Croatia, na baadae Uhispania itapambana na jamuhuri ya Irland.