Euro 2012

Ufaransa kuumana na wenyeji wa michuano ya Euro 2012 Ukraine

Timu ya taifa ya Ufaransa, les Blues, inashuka dimbani leo kuchuana na wenyeji wa michuano ya Euro 2012 Ukraine Kwenye uwanja wa Donbass Arena de Donetsk,. Ukraine wakiwa nyumbani watatamba katika mechi yao hiyo ya pili baada ya mechi ya kwanza kuishinda Swiden mabao 2-1. 

Matangazo ya kibiashara

Ufaransa iliotoka sare ya bao moja kwa moja na Uingereza katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo,, inatakiwa kufunga mechi hii ya pili ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea na michuano hiyo.

Ufaransa imekwisha kutana na Ukraine mara sita na haijawahi kufungwa na Ukraine. Imeishinda Ukraine mara tatu na imegawa mara tatu. Baada ya dakika 90, ndipo tutajuwa matokeo. Je Nurdine Ukraine watakubali kusindwa wakiwa Nyumbani?

Mechi nyingine katika kundi hili itazikutanisha Uingereza na Sweden. Uingereza kumbuka kwamba iligawa na Ufaransa bao 1-1 katika mechi yake ya kwanza huku Sweden ikifungwa na Ukraine bao 2-1 katika mechi yake ya kwanza. Itakuwa basi ni kindumbwe ndumbwe kila timu yahitaji ushindi.