LIGI KUU YA UINGEREZA

Ratiba ya Ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2012/2013 yatangazwa

Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2011/2012 manchester City
Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2011/2012 manchester City Reuters

Ratiba ya msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Backlays Premier League imetolewa hii leo na chama cha soka nchini humo FA ambapo kwa mujibu wa kalenda itaanza kutimua vumi kuanzia tarehe 18 ya mwezi wa 8 mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye ratiba hiyo mabingwa wapya Manchester City wanatarajia kufungua dimba na timu iliyopanda daraja msimu huu ya Southampton mchezo ambao Man City itakuwa mwenyeji.

Klabu ya Everton yenyewe itakuwa mwenyeji wa timu ya Manchester United ambao msimu uliopita walishuhudiwa wakiutema ubingwa wa nchi hiyo kwa majirani zao Man City.

washika bunduki wa jiji la London klabu ya Arsenal watakuwa nyumbani kwenye dimba lao la Emirates kuwakaribisha vijana wa Sunderland ambao msimu uliopita ilikuwa tishio kwa vigogo.

Newcastle United ambao msimu uliopita nao walikuwa tishio, wao watakuwa wenyeji wa timu ya Tottenham Hotspurs ambao walimaliza kwenye nafasi ya nne kwenye msimu wa ligi ulioisha huku msimu huu pia ikitarajiwa kuwa tishio.

Mabingwa wa Ulaya klabu ya Chelsea wao watakuwa wageni wa klabu ya Wigan kwenye mchezo ambao utashuhudia klabu hiyo ikiwa chini ya kocha wake aliyekuwa wa muda na kupewa kibarua cha miaka miwili De Matteo.

Tayari homa ya kuanza kwa ligi hiyo imeanza kupanda kwa mashabiki wa soka huku wakisubiri kuona wachezaji ambao wamesajiliwa na timu zao kwaajili ya msimu huu wa ligi.