US OPEN

Webb Simpson ndiye bingwa wa michuano ya US Open 2012

Webb Simpson bingwa wa michuano ya US Open 2012
Webb Simpson bingwa wa michuano ya US Open 2012 Reuters

Michuano ya Golf ya US Open hatimaye imemalizika hapo jana jioni na kushuhudia Mmarekani Webb Simpson akitwaa taji hilo.

Matangazo ya kibiashara

Mashindano hayo ambayo yalihusisha wachezaji maarufu wa mchezo huo akiwemo Tiger Woods na Lee Westwood ambao hata hivyo hawakufua dafu kwenye michuano ya mwaka.

Kwenye mzunguko wa kwanza na wa pili ilishuhudiwa wachezaji Tiger Woods akifanya vema na kudhaniwa anegeweza kuibuka na ushindi kwenye michuano ya mwaka huu lakini ndoto zake ziligonga mwamba baada ya kushindwa kufungwa kwenye mashimo mengi.

Akizungumzia ushindi wake Simpson amesema kuwa hakutarajia kama angeibuka na ushindi kwenye mashindano ya mwaka huu lakini kwakuwa alijiamini na alikuwa mmoja wa washindani alijidhatiti na kufanikiwa kuchomoza na ushindi.

Kwa upande wake Tiger Woods ambaye amerejea kwenye kiwango chake hivi karibuni amekiri michuano ya mwaka huu kuwa mgumu lakini anashukuru kwa kumaliza kwenye nafasi nzuri na kwamba anatarajiwa kufanya vizuri zaidi kwenye michuano ijayo.