EURO 2012

Uingereza na Ufaransa zatinga robo fainali ya michauno ya Euro 2012, robo fainali ya kwanza kupigwa Alhamisi

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wakimpngeza Wyne Rooney baada ya kuifungia timu yake goli dhidi ya wenyeji Ukrain
Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wakimpngeza Wyne Rooney baada ya kuifungia timu yake goli dhidi ya wenyeji Ukrain Reuters

Michuano ya kombe la mtaifa ya Ulaya Euro 2012 imetinga kwenye hatua ya robo fainali baada ya kukamilishwa kwa ratiba ya mechi zilizokuwa zimesalia hapo jana na kuhsuhudia timu ya taifa ya Uingereza na Ufaransa zikitinga kwenye hatua hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Timu ya taifa ya Uingereza hapo jana ilikuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Ukrain ambayo ni mwenyeji wa mcuhiano na kushuhudia wenyeji Ukrain wakiaga michuano hiyo kwa kukubali kipigo cha bao 1-0.

Bao la timu ya taifa ya Uingereza lilifungwa na mshambuliaji Wyne Rooney ambaye ilikuwa ni mechi yake ya kwanza toka arejee uwanjani baada ya kutmikia kutocheza mechi tatu za michuano hiyo.

Kabla ya mchezo huo kocha Roy Hodgson alimtabiria mema mchezaji huyo akimtaja kama mwenye bahati na kwamba angeweza kufunga goli jambo ambali lilifanyika.

Kwenye mchezo mwingine timu ya taifa ya Sweden walikuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa kwenye mchezo ambao umeshuhudia Sweden wakiibuka na ushindi wa mabo 2-0.

Magoli ya Zlatan Ibrahimovic na Sebastian Larsson yalitosha kuzamisha jahazi la Ufaransa ambalo chupuchupu lingeweza kuaga michuano hiyo iwapo Sweden wangepata mabao matatu.

Robo fainali ya kwanza itachezwa siku ya Alhamisi ambapo timu ya taifa ya Jamhuri ya Cheki itakuwa mwenyeji wa timu ya taifa ya Ureno, wakati siku ya Ijumaa Ujerumani watakuwa mwenyeji wa Ugiriki.

Siku ya Jumamosi timu ya taifa ya Hispania itakuwa na kibarua dhidi ya Ufaransa wakati siku ya Jumapili timu ya taifa ya Uingereza itakuwa mwenyeji wa Italia.