EURO 2012

Timu za Ureno na Jamhuri ya Czech kukutana leo kwenye robo fainali ya kwanza ya michuano ya Euro 2012

wachezaji wa timu ya taifa ya Ureno wakiwa kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo wa leo
wachezaji wa timu ya taifa ya Ureno wakiwa kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo wa leo Reuters

Kindumbwendumbwe cha robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya, Euro 2012 kinatarajiwa kuanza kutimua vumbi hii leo kwa timu za taifa za Ureno na Jamhuri ya Czech zitakapopambana.

Matangazo ya kibiashara

Hapo jana ilikuwa ni mapumziko ambapo hii leo sasa timu zitaanza kushuka dimbani kupambana kwenye mchezo wa robo fainali ambapo hii inakuwa ni robo fainali ya kwanza.

Mchezo huo ambao tayari umevuta hisia za mashabiki wengi wa soka barani Ulaya, unatarajiwa kuwa wa kuvutia hasa kutokana na aina ya mchezo ambao timu zote mbili zinacheza huku Jamhuri ya Czech ikipewa nafasi ya kuibuka na ushindi.

Wachambuzi wa soka wanaipa nafasi kubwa Jamhuri ya Czech kuibuka na ushindi kwenye mechi ya leo ingawa wanadai lolote linaweza kutokea kwakua Ureno ilionyesha utofauti mkubwa kwenye mechi za kumaliza za makundi.

Mchezaji Christian Ronaldo anatajwa kuwa chachu ya ushindi wa timu ya taifa ya Ureno kwenye mchezo wa hii leo.