NEW YORK-MAREKANI

Shirikisho la mchezo wa ngumi duniani la WBO lasema bondia, Manny Pacquiao alishinda kwenye pambano lake na Timothy Bradley

Bondia Manny Pacquiao akirusha konde kwa mpinzani wake Timothy Bradley (kushoto)
Bondia Manny Pacquiao akirusha konde kwa mpinzani wake Timothy Bradley (kushoto) Reuters

Hatimaye bondia wa Ufilipino Manny Pacquiao amefanikiwa kurejesha taji lake la ubingwa wa dunia la WBO alilopoteza mwezi uliopita nchini Marekani kwenye pambano lake na Timothy Bradley.

Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa Pacquiao umetangazwa na jopo la majaji wa kimataifa waliotwa na shirikisho la dunia la mchezo huo kupitia upya mkanda wa veideo wa pambano kati ya bondia huyo na Bradley ambaye majaji walimpa ushindi Bradley kwa alama 115-113.

Taarifa ya shirikisho la mchezo huo, imesema kuwa baada ya kujiridhisha na mchezo mzima ni wazi kuwa majaji walifanya makosa kwenye kutoa maamuzi kuhusu ambano hilo kwani bondia Manny Pacquao alirusha ngumi nyingi kuzidi mpinzani wake.

Japo jopo la majaji watano wameamua vinginevyo lakini shirikisho la WBO halina uwezo wa kutengua maamuzi ya awali ila kinachowezekana ni kuitishwa kwa pambano la marudiano kati ya mabondia hao wawili.

Mara baada ya mchezo wake na Bradley kutangazwa mshindi mashabiki waliokuwa wamefurika kushuhudia mchezo huo walianza kuzomea uamuzi wa majaji kwa kumpa ushindi Bradley.