EURO 2012

Ureno yawa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya Euro, leo ni zamu ya Ujerumani na Ugiriki kumenyana

Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya taifa ya Ureno Christina Ronaldo akishangilia mara baada ya mchezo wa jana
Mshambuliaji wa pembeni wa timu ya taifa ya Ureno Christina Ronaldo akishangilia mara baada ya mchezo wa jana Reuters

Robo fainali ya pili ya michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya, Euro 2012 inatarajiwa kutimua vumbi hii leo baada ya hapo jana kushuhudia timu ya taifa ya Ureno ikitinga kama timu ya kwanza kwenye hatua ya nusu fainali.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye mechi ya jana, timu ya taifa ya Ureno ilicheza na Jamhuri ya Czech kwenye mchezo ambao ulishuhudia upinzani mkali kwa timu zote mbili.

Christian Ronaldo ndie aliyepeleka kilio kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech baada ya kuunganisha pasi nzuri toka kwa Luis Nani na kupiga kichwa mpira ambao ulimshinda mlinda mlango Peter Czeck.

Mara baada ya mchezo winga huyo wa Ureno hakusita kuwapongeza wachezaji wake kwa kiwango walichokionyesha na nia ya kutaka kushinda kwenye mchezo huo jambo ambalo walilifanikisha.

Hii leo kwenye robo fainali nyingine, timu ya taifa ya Ujerumani itakuwa ikipepetana na timu ya taifa ya Ugiriki kwenye mchezo ambao Ujerumani inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo.

Wachambuzi wa masuala ya soka wanaona kuwa licha ya Ujerumani kuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo lakini pia Ugiriki wanao nafasi hasa kutokana na aina ya mchezo ambao timu hizo zinacheza.