UKRAINE

Uingereza yaondolewa katika mashindano ya Euro 2012.

Wachezaji wa Italy baada ya kumalizika kwa muda wa ziada bila kufungana.
Wachezaji wa Italy baada ya kumalizika kwa muda wa ziada bila kufungana. bleacherreport.com

Timu ya Soka ya Uingereza imeondolewa katika mashindano ya Euro 2012, baada ya kukubali kichapo cha magoli 4-2 kutoka kwa Italia usiku wa Jumapili katika mchezo wa robo fainali uliofanyika mjini Kiev nchini Ukraine. 

Matangazo ya kibiashara

Magoli hayo manne yalipatikana baada ya kumalizika kwa dakika thelathini za muda wa ziada huku timu hizo zikishindwa kufungana hivyo kuingia katika hatua ya mikwaju ya penalti.

Alessandro Diamanti alifunga bao la kuamua mshindi katika mikwaju hiyo ya penalti, baada ya Ashley Young na Ashley Cole kukosa kufunga mabao kupitia mikwaju waliyopiga.

Italia sasa itapambana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali itakayochezwa siku ya Alhamisi huko Warsaw nchini Poland.