UINGEREZA

Nadal,Kvitova waanza harakati za kampeni za Wimbledon

Rafael Nadal,moja kati ya wachezaji wa Tenis wanaotarajiwa kutamba katika michuano ya Wimbledon
Rafael Nadal,moja kati ya wachezaji wa Tenis wanaotarajiwa kutamba katika michuano ya Wimbledon REUTERS/Regis Duvignau

Mcheza tennis mahiri kwa upande wa wanaume Rafael Nadal na bingwa mtetezi kwa upande wa akina dada Petra Kvitova wanaanza harakati zao za kampeni za wimbledon jumanne wakati wakongwe Andy Roddick na Lleyton Hewitt wakianza wimbi la kuunga mkono harakati hizo.

Matangazo ya kibiashara

Nadal,ambaye amevunja rekodi saba katika michuano ya French Open atamkabili raia wa Brazil Thomas Bellucci mara baada ya Kvitova ambaye alishinda taji mwaka jana kukabiliana na Akgul Amanmuradova wa Uzbekstan.

Wakati huhuo raia wa Uingereza Andy Murray, ambaye ameibuka katika nusu fainali mbili katika kipindi cha miaka miwili iliyopita atavaana na raia kutoka Urusi Nikolay Davydenko.

Lleyton Hewitt, ambaye aliibuka bingwa mwaka 2002 lakini bado anahitaji uwanja mpana kucheza mwaka huu anakabiliwa na mchezaji kutoka Ufaransa Jo-Wilfried Tsonga, ambaye alimgaragaza Roger Federer katika michuano ya kuelekea nusu fainali mwaka jana.

Naye Roddick, ambaye ameibuka mara tatu anaingia uwanjani dhidi ya Jamie Baker ambaye aliibuka kifua mbele juma lililopita katika michuano ya Eastbourne.